Shirika la Fedha Duniani (IMF) linajumuisha nchi 188; na lengo lake kuu ni kuleta utulivu wa kifedha duniani.
Kazi kubwa ya Shirika la IMF ni kzisaidia nchi zinazokabiliana na hatari ya kufilisika. Makao yake makuu yapo mjini Washington, Marekani. Mkurugenzi mtendaji wa shirika hili kwa sasa ni Christine Lagarde, waziri wa fedha wa zamani wa Ufaransa.