ICJ yakataa ombi la kuizuwia Ujerumani kuipa silaha Israel
30 Aprili 2024Matangazo
Kwenye kesi ya msingi katika mahakama hiyo ya juu kabisa ya Umoja wa Mataifa, Nicaragua ilikuwa inaituhumu Ujerumani kwa kusaidia mauaji ya halaki huko Gaza kwa kuipatia silaha Israel.
Katika ombi lake lililowasilishwa tarehe Mosi Machi, Nikaragua ilihoji kwamba kwa kuipatia Israel msaada wa kisiasa, kifedha na kijeshi na kuondosha ufadhili wake kwa Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia Wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA, Ujerumani inawezesha utendwaji wa mauaji ya kimbari na imeshindwa kutimiza wajibu wake wa kuyazuwia.
Soma zaidi: Ujerumani yajitetea katika mahakama ya ICJ
Hata hivyo, mkuu wa ujumbe wa Ujerumani kwenye mahakama hiyo, Tania von Uslar-Gleichen, aliyaita madai hayo kuwa hayana msingi wowote wa kisheria.