1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

ICJ - Mahakama ya kimataifa ya haki

ICJ ni mahakama ya Kimataifa ya Haki ambayo pia inajulikana kwa jina la Mahakama ya Dunia, ni sehemu ya Umoja wa Mataifa.

Makao yake makuu ni mjini The Hague, Uholanzi. Kazi zake kuu ni pamoja na kusuluhisha mizozo ya kisheria inayowasilishwa na nchi wanachama wake – mara nyingi huwa inashughulikia mizozo inayohusu mipaka ya nchi pamoja na migogoro ya rasilimali za nchi. Mahakama hii pia inafanya kazi ya kutoa ushauri juu ya masuali ya kisheria yanayowasilishwa na mashirika ya kimataifa pamoja na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa.