HEILIGENDAMM: Maandamano nchini Ujerumani kupinga utandawazi. | Habari za Ulimwengu | DW | 02.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

HEILIGENDAMM: Maandamano nchini Ujerumani kupinga utandawazi.

Waandamanaji waliojifunika nyuso zao wamevunja madirisha, wakavurumisha mawe pamoja na chupa huku polisi wakitumia fimbo kuwatawanya kwenye mji wa bandari wa Rostock, kaskazini mwa Ujerumani.

Ghasia hizo zimezuka baada ya maandamano yaliyoarifiwa kuwa ya utulivu katika mji huo.

Kundi la waandamanaji limewashambulia polisi ambao wamejibiza kwa kurusha mabomu ya kutoa machozi.

Watu kadhaa wametiwa nguvu.

Duru zinasema watu kiasi 2,000 walijumuika mjini Rostock wakipinga mkutano wa juma lijalo wa mataifa manane yaliyostawi kiviwanda, G8, katika mji wa kitalii wa Heilegendamm.

Serikali ilikuwa imepiga marufuku maandamano yaliyopangwa na kundi la manazi mambo-leo katika mji wa karibu wa Schwerin ambayo yalidhamiriwa kuwa wakati sawa na maandamano ya wapinga utandawazi.

Hatua hiyo imechukuliwa kwa kuchelea ghasia kuzuka.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com