Hali wilayani Bududa, Uganda baada ya maporomoko ya ardhi | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 04.03.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Hali wilayani Bududa, Uganda baada ya maporomoko ya ardhi

Juhudi za kutafuta miili ya watu waliofariki kutokana na maporomoko ya ardhi wilayani Bududa nchini Uganda bado zinaendelea, licha ya kukumbwa na changamoto kadhaa, ikiwemo uduni wa vifaa wanavyotumia.

Waokoaji wapo kazini kutafuta miili ya watu

Waokoaji wapo kazini kutafuta miili ya watu

Hali hiyo pia inatokana na ukosefu wa barabara za kupitisha mashine nzito kama vile greda.

Mwandishi wetu nchini Uganda, Leylah Ndinda, ambaye ametembelea eneo hilo, anaarifu kuwa shughuli za uchimbaji zilisitishwa jana jioni na mvua kubwa iliyonyesha, hali iliyosababisha watu kulimbia eneo la tukio wakihofia

kutokea tena kwa maporomoko ya ardhi.

Leylah Ndinda anaeleza zaidi hali ilivoyo kwa sasa katika eneo hilo.

Mwandishi: Leyla Ndinda Mhariri: Othman Miraji

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com