GAZA: ripota wa BBC bado ashikiliwa na wateka nyara | Habari za Ulimwengu | DW | 16.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA: ripota wa BBC bado ashikiliwa na wateka nyara

Shirika la utangazaji la Uingereza BBC limo katika wasi wasi mkubwa juu ya ripota wake Alan Johnston. Kundi linalojiita Al Tawhid Al Jihad limedai kuwa limemwuua mwandishi huyo.Lakini habari hizo hizijathibitishwa.

Bwana Johnston alitekwa nyara mapema wiki jana alipokuwa anarejea nyumbani kutoka kwenye ofisi yake iliyopo kwenye Ukanda wa Gaza.

Wizara ya mambo ya nje ya Uingereza imesema inafuatilia kwa makini mkasa wa mwandishsi huyo ambae ni miongoni mwa maripota wachache kutoka nchi za magharibi ambao bado wanafanya kazi kwenye Ukanda wa Gaza.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com