GAZA: Mashambulio ya Israel yameua Wapalestina 6 | Habari za Ulimwengu | DW | 18.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA: Mashambulio ya Israel yameua Wapalestina 6

Ndege za kivita za Israel tena zimeshambulia Ukanda wa Gaza na kuuwa Wapalestina 6.Mashambulio hayo mapya yalilenga gari lililokuwa likivuka mpaka kati ya Israel na kusini mwa Ukanda wa Gaza.Hapo awali mashambulio ya angani yalipiga jengo lililokuwa likitumiwa na Hamas.Katika shambulio hilo mtu mmoja aliuawa na 40 wengine walijeruhiwa.Maafisa wa usalama wa Kipalestina wamesema kama vifaru 15 vya Kiisraeli vimeingia Ukanda wa Gaza.Kwa mujibu wa maafisa wa Kiisraeli,operesheni zao za kijeshi zimelenga wanamgambo waliokuwa wakivurumisha makombora dazeni kadhaa kusini mwa Israel,tangu siku tatu zilizopita.Kwa upande mwingine mapambano kati ya makundi hasimu ya Kipalestina ya Hamas na Fatah yameendelea licha ya kufanywa jitahada nyingi za kusitisha mapigano hayo.Hadi watu 40 wameuawa tangu mapigano kati ya pande hizo mbili kuanza upya mwisho wa juma lililopita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com