GAZA CITY: Mashambulio ya Israel yameua Wapalestina
13 Oktoba 2006Shambulio la jeshi la anga la Israel katika mtaa wa Gaza wenye wakazi wengi,limeua wanamgambo 2 na mtoto mmoja.Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya madaktari wa Kipalestina.Alkhamisi usiku,ndege ya Kiisraeli ilirusha makombora kwenye nyumba inayoaminiwa kuwa ya kamanda wa Hamas wa ngazi ya juu.Madaktari katika mtaa huo wamesema,wametoa matibabu kwa watu 7 waliojeruhiwa katika shambulio hilo,miongoni mwao wakiwepo watoto wengi.Wakazi wa eneo hilo wamesema,onyo linalotolewa kwa kawaida kuwataka watu watoke majumbani mwao,safari hii halikutolewa na jeshi la Kiisraeli.Katika uvamizi wa mapema Alkhamisi asubuhi,vifaru vya Kiisraeli viliingia kusini mwa Gaza kupambana na wanamgambo waliokuwa wakikusanyika katika eneo hilo.Ndege za Kiisraeli zilirusha makombora mawili na kuwaua Wapalestina 6,ikiwa ni pamoja na mtoto wa kiume wa miaka 14.