Finali ya Kom,be la Afrika:Ghana na J.K.Kongo Abidjan | Michezo | DW | 06.03.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Finali ya Kom,be la Afrika:Ghana na J.K.Kongo Abidjan

Kombe litaelekea wapi jumapili ?

Hatima ya Klinsmann ?

Hatima ya Klinsmann ?

Kesho (jumapili) ni finali ya Kombe la Afrika la Mataifa kwa wachezaji wa nyumbani Afrika ni kati ya Jamhri ya Kidemokrasi ya Kongo na Ghana huko Abidjan,Corte d Iviore- Mabingwa wa Ujerumani-Bayern Munich wataondoka uwanjani na ushindi dhidi ya Hannover leo (jumamosi) au wameahidiwa pigo jengine na wageni wao Hannover baada ya pigo la juzi la mabao 4-2 huko Leverkusen ?

Kombe la Afrika:Macho ya mashabiki wa dimba barani Afrika yanakodolewa Abidjan,Ivory Coast,. mwishoni mwa wiki hii kujionea vipi finali ya Kombe hilo kwa wachezaji wanaosakata dimba Afrika itamalizika: Taifa Stars-Tanzania ilikuwa mojawapo ya timu zilizoshiriki katika kombe hilo nchini Corte d-Iviore,lakini baada ya kumudu sare tu ya bao 1:1 na Chipolopolo-Zambia juzi jumatano, safari ya kurudi Tanzania,haikuepukika na Taifa Stars walifunga virago haraka wakingoja kujua hatima ya majirani zao Chipolopolo-Zambia inayoania nafasi ya 3 leo .

BUNDESLIGA:

Ligi mashuhuri barani Ulaya mwishoni mwa wiki hii: Bundesliga iko uwanjani na swali la kila shabiki- ni je, mabingwa Munich watateleza tena leo kama jumapili iliopita walipocheza na Bremen na kumudu sare 0:0 au kati ya wiki walipozabwa mabao 4-2 na Leverkusen katika kombe la DFB-shirikisho la dimba la Ujerumani ?

Kocha wa Bayern Munich Juergen klinsmann, akiwa amejipatia ushindi m ara moja tu katika mechi 5 zilizopita mwaka huu,alepelekewa salamu za kuwa na imani nae na meneja wa Bayern munich,Uli Hoeness hapo juzi. Kwani, Klinsmann amekuwa hamkani kabisa baada ya timu yake bingwa kuangukia safu ya 5 ya ngazi ya Bundesliga na kuvuna pointi 4 kati ya 15 ilizoania tangu mwaka mpya kuingia.

Kutoka suluhu ya 0:0 jumapili iliopita na mahasimu wao Werder Bremen waliocheza na wachezaji 10 tu tangu dakika ya 15 ya mchezo, kulipiga msumari wa moto juu ya donda la Klinsmann.Hata ule ushindi wa mabao 5-0 katika Champions League-kombe la klabu bingwa barani Ulaya dhidi ya sporting Lisbon, haukumsaidia Klinsmann kutolaumiwa.

Bayern Munich ikiwa uwanjani wakati huu ikicheza nyumbani na Hannover,haidiriki tena kushindwa.Kikawaida dhidi ya timu kama Hannover iliopo safu ya kati ya Ligi ni chapati kwa mabingwa.Lakini, hata FC Cologne, iliopo safu kama hiyo, ilithubutu kutamba mjini Munich na kutoroka sio tu na jogoo lao Lukas Podolski mwisho mwa msimu huu, bali hata na pointi 3. Ni katika hali hii changamoto hii iliopo uwanjani hivi sasa na Hannover inaangaliwa. Mimi nisingethubutu kuagua firimbi ya mwiosho italiaje licha ya kwamba Hannover iko nafasi ya 12 katika ngazi ya Ligi.

Hata stadi wao mfaransa Franck Ribery, amekuwa akinungunika karibuni akidai akiongoza hujuma usoni, hasaidiwi na wenzake.Ribery kwakweli ndie mashini ya Bayern Munich,bila ya machachari yake usoni,akina Luca Toni na Miroslav Klose ni vigumu kutia magoli.

Hamburg iliopo nafasi ya pili ya ngazi ya Ligi nyuma ya Hertha Berlin,imefunga safari jioni hii kuitembelea Borussia Moenchengladbach ambayo inauburura mkia wsa Ligi.Hoffenheim,chipukizi waliotoka daraja ya pili ya Bundesliga msimu huu na kuhanikiza kwa dimba lao hadi kileleni mwa Ligi, wamerudi nyuma nafasi ya 3 .Hivi sasa lakini wanatamba nyumbani mbele ya Werder Bremen.

Premier League -ligi ya Uingereza, Sunderland ina miadi jioni hii na Tottenham Hotspur wakati mabingwa Manchester United wanacheza katika robo-finali ya Kombe la FA na Fulham.Manu inalenga kutwaa vikom,be vyote 5 msimu huu tangu vya nyumbani hata vya ugenini. Mahasimu wao waliorudi kupata nguvu tangu kuongozwa na kocha mdachi-Guus Hiddink,wanapambana na Coventry.

Katika La Liga au ligi ya Spain, viongozi wa muda mrefu wa Ligi hiyo-FC Barcelona wanapambana jioni hii na Athletico Bilbao.Ingawa Barca wanacheza nyumbani,hakuna uhakika wa kuondoka na pointi 3.kwani, wakiongoza muda mrefu kwa pointi 12 na sasa mwanya wao umepunguzwa na mabingwa Real hadi pointi 4.Wakiteleza tena leo,basi stahili yao.Mahasimu wao Real Madrid pia wanacheza nyumbani katika vita vya ndugu wawili-Real na Atletico Madrid. Villareal wamejinoa tayari kuwanyakua Espanyol.Ukiwa ni shabiki wa Serie A-Ligi ya Itali, usiwe na wivu,kwani tunawachukua pia huko.

As Roma inaumana na Udinese wakati Genoa imejinoa kuinyoa Inter Milan.Hatima ya Juventus itajulikana leo huko Torino.AC Milan na mastadi wake akina Ronaldinho na kaka, inabidi kusubiri hadi jumapili kuwachangamsha mashabiki wa Atalanta Bergamo .catania inacheza na Siena wakati Fiorentina ina miadi pia kesho na Palermo.Napoli wamewaalika nyumbani kuwaburudisha kwa dimba Lazio Roma.