Finali ya Kombe la Afrika chini ya umri 20 | Michezo | DW | 30.01.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Finali ya Kombe la Afrika chini ya umri 20

Nani ataondoka kesho na Kombe Kigali:Kamerun au Ghana ?

default

Munich na Hoffenheim (hapo)

Baada ya likizo ya x-masi na mwaka mpya,Bundesliga-ligi ya Ujerumani, imerudi uwanjani jana kwa kishindo baada ya mabingwa Bayern Munich kufungua duru ya pili ya msimu na mahasimu wao wa kaskazini Hamburg.

Jioni ya leo (Jumamosi) ni zamu ya viongozi wa ligi-chipukizi waliotoka daraja ya pili Hoffenheim wakiwa na miadi na Cottbus.

Kesho "asie na mwana aeleke jiwe na asie na mguu atie gongo-mkutano mjini Kigali" -finali ya Kombe la vijana la Afrika chini ya umri wa miaka 20 baina ya Simba wa nyika-Kamerun na Ghana.

Baada ya dada wa wili akina Serena na Venus Williams kutwaa taji la Tennis la ubingwa wa Australian Open la wawili-wawili(Double),leo Serena anatapia taji la pili katika finali na mrusi Dinara Safina.

Tuanze na finali ya Kombe la afrika la vijana chini ya umri wa miaka 20 mjini Kigali,Ruanda.Baada ya Kamerun kuwapiga kumbo mabingwa mara 5 Nigeria na Ghana kuzima vishindo vya Afrika kusini,mlango ni wazi sasa kwa finali ya kesho kati ya Kamerun na Ghana.Kombe litaelekea wapi ?

Bundesliga imerudi uwanjani kwa duru ya pili ya msimu jana pale mabingwa Bayern Munich walipowatembelea mahasimu wao wa kaskazini Hamburg.

Macho ya mashabiki lakini,yanakodolewa changamoto za leo na hasa chipukizi waliotoka daraja ya pili na kuongoza Bundesliga-Hoffenheim ambao jioni ya leo, wana miadi na Cottbus.Jogoo lao lililotia mabao 18 katika duru ya kwanza ya msimu huu,mbosnia Vedad Ibisebic limeumia na halitarudi uwanjani tena alao msimu huu.Kujaza pengo lake, Hoffenheim imeliazima jogoo la Kamerun anaeichezea Bremen, Boubacar Sanogo.

Hertha Berlin, inayosimama nafasi ya tatu ya ngazi ya Bundesliga,iko nyumbani leo ikiikaribisha Eintracht Frankfurt.

Changamoto nyengine za Bundesliga leo ni kati ya FC Cologne na Wolfsburg wakati Bayer Leverkusen ina miadi na Borussia Dortmund. Macho pia yatakodolewa leo mpambano baina ya Schalke na Hannover wakati Stuttgart inakumbana na Borussia Monchengladbach.

Werder Breme iliowavunja moyo mashabiki wake duru ya kwanza ya msimu wanatumai kutamba kesho mbele ya Bielefeld wakati Bochum inacheza na Karlsruhe.

Katika Premier League-ligi ya Uingereza,mabingwa Manchester United wanarudi uwanjani wakiwa na pointi 2 usoni kileleni mbele ya Liverpool na Chelsea zenye miadi kesho.Aston villa iko nyuma kwa pointi 1.Ikitegemea matokeo baina ya Manu na Aston Villa,Chelsea na Liverpool zaweza zikaangukia nafasi ya tatu na ya 4 kabla firimbi kulia kesho jumapili.Kwa kumudu sare tu katika mechi zake 3 zilizopita, Liverpool inabidi kutamba kwani iko sasa nafasi ya 3 kutoka ya kwanza.

Katika Seria A,Ligi ya itali,ushindi nyumbani kesho dhidi ya Torino inayopepesuka utaimarisha nafasi yao Inter Milan kileleni wakati Juventus iliopo nafasi ya pili itatokwa na jasho leo kabla kuweza kutamba dhidi ya cagliari na AC Milan wakipambana na Lazio kesho jioni.Napoli inakumbana na Udinese leo wakati Atalanta na Catania wanaonana kesho.

Katila la Liga-ligi ya Spian, FC Barcelona watasaka kesho ushindi wao wa 9 mfululizo watakapoonana na Racing Santander.Barcelona wamekuwa wakivunja rekodi zote msimu huu n a shabaha yao ni kuvunja rekodi ya magoli 107 iliowekwa na mahasimu wao Real msimu wa 1989/90.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com