DUSHENBE: Rais Rakhmonov aibuka mshindi katika uchaguzi wa urais wa Tajikistan | Habari za Ulimwengu | DW | 07.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

DUSHENBE: Rais Rakhmonov aibuka mshindi katika uchaguzi wa urais wa Tajikistan

Rais anayeyaacha madaraka nchini Tajikistan, Emomali Rakhmonov, ameshinda na asili mia 76 ya kura katika uchaguzi wa urais na hivyo ataiongoza nchi kwa mhula wa miaka mingine 7 ijayo. Afisa moja wa tume ya uchaguzi amesema mpinzani aliyetoka wa pili Olimzhon Boboyev, amepata asili mia 7 tu. Asili mia 91 ya watu waliojiandikisha walipiga kura. Rais Rakhmonov alitupilia mbali lawama za wachunguzi wa nchi za magharibi ambao walilikosoa zoezi hilo la uchaguzi nchini Tajikistan. Rais Rakhmonov amesema uchaguzi ulikuwa wa kidemokrasi lakini akakiri kuwa haukufikia kiwango cha nchi za magharibi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com