DOHA:Zawahiri asema al-Qaeda itaendelea kulenga mashambulio yake dhidi ya Marekani na washirika wake | Habari za Ulimwengu | DW | 21.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

DOHA:Zawahiri asema al-Qaeda itaendelea kulenga mashambulio yake dhidi ya Marekani na washirika wake

Kiongozi nambari mbili wa mtandao wa kigaidi wa Alqaeda Ayman-Zawahiri amesema kundi hilo litaendelea kuilenga Marekani pamoja na nchi nyingine za Magharibi hadi pale mashambulizi dhidi ya waislamu yatakapokomeshwa.

Katika ukanda wa video uliorushwa hewani na kituo cha televisheni cha kiarabu cha Aljazeera Zawahiri pia amepinga hatua ya rais Mahmoud Abbas ya kutaka ufanyike uchaguzi wa mapema nchini Palestina.

Badala yake al Zawahiri amewaambia wapalestina kitakachowakomboa ni vita takatifu vya Jihad pekee.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com