1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dakar. Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani yuko nchini Senegal kwa mkutano wa uchumi wa bara la Afrika.

20 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEsb

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice amewasili nchini Senegal mwanzoni mwa ziara yake ya siku tano ambapo pia itaizuru Sudan na mashariki ya kati. Wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani imesema kuwa Rice atahudhuria mkutano wa uchumi wa bara la Afrika nchini Senegal kabla ya kwenda katika jimbo lililokumbwa na ghasia la Dafur nchini Sudan na kutembelea kambi ya wakimbizi.

Maafisa wamesema kuwa lengo kubwa la ziara yake ya mashariki ya kati itakuwa kuweka mpango wa Israel wa kujiondoa kutoka katika eneo la Gaza katika njia sahihi.

Wakati huo huo waziri huyo wa mambo ya kigeni wa Marekani amesema kuna uwezekano wa kumtuma balozi wa Marekani nchini Sudan kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1997 ikiwa ni ishara ya hali kuwa nzuri ya uhusiano baada ya serikali mpya kuingia madarakani mwezi huu.

Viongozi wa serikali ya muungano kwa ajili ya amani waliapishwa hapo Julai 9.