CRAWFORD: Rais George W Bush ashauriana na wakuu wa usalama wa Marekani | Habari za Ulimwengu | DW | 29.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

CRAWFORD: Rais George W Bush ashauriana na wakuu wa usalama wa Marekani

Rais wa Marekani George W Bush amesema amepiga hatua nzuri ya mkakati mpya kuhusu Iraq.

George Bush alikuwa akishauriana na wakuu wa usalama wa marekani huko Crawford, Texas.

Miongoni mwa waliohudhuriwa kikao hicho ni makamu wa rais, Dick Cheney, Waziri wa mambo ya nje, Condoleeza Rice na waziri mpya wa Ulinzi, Robert Gates.

Bush aliwelezea waandishi wa habari nia yake kushughulikia kwa dharura suala la Iraq

"Nimekutakana na wakuu wangu wa usalama. Hii ndio mara ya kwanza kwangu mimi kukaa pamoja na Waziri Gates tangu aliporudi kutoka Iraq. Jenerali Pace aliandamana na waziri Gates na wakatoa taarifa ya mambo yalivyo. Hiyo ni njia mwafaka ya kuhakikisha kutimia lengo letu Iraq"

Bush alisema ataendelea na mashauriano kuhusu Iraq na kwamba serikali yake itawasiliana na wabunge wa Bunge la Congress.

Rais huyo wa Marekani anatarajiwa kuzindua mkakati wake mpya wa Iraq mwezi ujao.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com