Chama tawala CCM nchini Tanzania kimeridhia kuundwa serikali ya mseto visiwani Zanzibar | Matukio ya Kisiasa | DW | 16.02.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Chama tawala CCM nchini Tanzania kimeridhia kuundwa serikali ya mseto visiwani Zanzibar

Halmashauri ya taifa ya chama tawala cha Mapinduzi, CCM, huko Tanzania ilikutana kwa faragha kwa siku mbili huko Dodoma hadi jana usiku.

Na kati ya mambo yaliokabiliwa na kikao hicho kuyajadili ni hali ya kisiasa Visiwani Zanzibar baada ya Baraza la wawakilishi visiwani humo, kwa kauli moja, kulikubali pendekezo la kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa, na pia ripoti ya kamati ya chama hicho ilioundwa kusuluhisha tofauti zilizochomoza kati ya wabunge wa chama hicho baina ya wale wanaotajwa kupinga ufisadi na wale wanaotuhumiwa kuuendeleza ufisadi.

Othman Miraji amezungumza kwa njia ya simu na John Chiligati ambaye ni katibu mwenezi na itikadi wa Chama cha CCM. Kwanza anaelezea hivi kilichokubaliwa huko Dodoma jana kuhusu maridhiano ya Zanzibar...

Mahojiano :Othman Miraji/John Chiligati

Mhariri: Mohamed Abdulrahman

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com