1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha upinzani chashinda uchaguzi Thailand

3 Julai 2011

Upande wa upinzani umeibuka na ushindi wa uchaguzi wa bunge nchini Thailand

https://p.dw.com/p/11oEw
Mkuu wa chama cha upinzani Phue Thai party Yingluck ShinawatraPicha: AP

Wapiga kura wa Thailand wamelichagua bunge jipya.Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi na baada ya kuhesabiwa zaidi ya asili mia 92 ya kura,chama cha upinzani cha Puea Thai kinaongoza- kimejikingia viti 260 kati ya 500 vya bunge.Mgombea mkuu wa upande wa upinzani ni Yingluck Shinawatra,ambae ni dada wa Waziri Mkuu Thaksin Shinawatra aliyepinduliwa mwaka 2006.Mwanasiasa huyo tajiri anaishi uhamishoni Dubai.Thaksin Shinawatra ndie anaewaongoza wafuasi wa upande wa upinzani mashuhuri kwa jina-"Mashati mekundu."Waziri mkuu Abhisit Vejjajiva ambae chama chake cha Democratic kimejikingia viti 163 amekiri kwamba wameshindwa.

Wahlen in Thailand
Wananchi wakiteremka kwa wingi kupiga kuraPicha: AP

"Matokeo ni bayana-Puea Thai wameshinda,amesema Waziri Mkuu huyo anaemaliza wadhifa wake na kusisitiza "wanachokitaka ni umoja na suluhu" nchini.Yingluck Shinawatra,mwenye umri wa miaka 44 amesema ameshawasiliana na chama kimoja kidogo ili kuunda serikali ya muungano.