CEBU, PHILIPPINES: Mataifa ya kusini mashariki mwa Eshia yatwaa dhamana kwa kushirikiana na Burma. | Habari za Ulimwengu | DW | 14.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

CEBU, PHILIPPINES: Mataifa ya kusini mashariki mwa Eshia yatwaa dhamana kwa kushirikiana na Burma.

Mataifa ya kusini mashariki mwa Eshia yamekubali kutwikwa lawama kwa kushirikiana na serikali ya Burma huku yakiahidi kukabiliana nayo.

Mataifa kumi wanachama wa Umoja wa Mataifa ya Kusini mwa Eshia, yametoa taarifa katika kikao chao cha kila mwaka wakiwataka watawala wa kijeshi nchini Burma kuwachia huru wafungwa wote wa kisiasa na kuanzisha mashauriano na makundi yote yanayohusika nchini humo.

Mataifa hayo pia yametia saini mkataba kati yao na China kuhusu kuimarishwa biashara na huduma na hivyo kutoa nafasi ya kuanzishwa mwafaka wa biashara huru.

Viongozi wa mataifa hayo wametoa wito kwa wafadhili wa kimataifa kusamehe kwa muda nchi maskini madeni na badala yake kutumia fedha hizo kukabiliana na umaskini.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com