Bush alaani kisa cha Ghuba la Uajemi | Habari za Ulimwengu | DW | 09.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Bush alaani kisa cha Ghuba la Uajemi

WASHINGTON:

Rais George Bush wa Marekani amelaaani tukio la mataboti za Iran pamoja na meli za Marekani.

Kabla ya kuanza safari yake ya mashariki ya Kati,Bush amekiita kisa hicho kama cha kiuchokozi ambacho Iran isingekifanya.Mkanda wa Video umetolewa na serikali ya Marekani ukionyesha tukio hilo.Picha zinaonyesha mataboti za Iran zikikabiliwa na manuari za kijeshi za Marekani katika ghuba la Uajemi.Sauti katika mkanda huo inasikika ikitoa tisho kuwa meli za Marekani zinakwenda kulipuka. Picha hizo zilichukuliwa na mbaharia mmoja kutoka meli ya Marekani ya Destroyer.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com