1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Tanzania lajiandaa kupitisha sheria ya watu wenye ulemavu

Charo Josephat5 Mei 2009

Sheria hiyo inatarajiwa kuboresha ulinzi wa watu wenye ulemavu na utoaji wa huduma msingi

https://p.dw.com/p/Hk5j
Rais wa Tanzania Jakaya KikwetePicha: AP Photo

Serikali ya Tanzania imeaanda mswada wa sheria ya haki na maendeleo ya watu wenye ulemavu nchini humo. Mswada huo utawasilishwa bungeni na kujadiliwa kabla kupitishwa kuwa sheria itakayosaidia kuwalinda zaidi watu wenye ulemavu wa aina yoyote ile nchini Tanzania pamoja na kuboresha utoaji wa huduma msingi kwa watu hawa.

Sikiliza mahojiano kati ya Josephat Charo na mheshimwa Margaret Mkanga, mbunge viti maalum kundi la watu wenye ulemavu Tanzania, kuhusu mswada huo. Kwanza anaeleza hisia zake kuhusu mswada huo.