BRUSSELS: Ufaransa kuyatambua mauaji ya Waarmenia kuwa ya kimbali kuazua wasi wasi | Habari za Ulimwengu | DW | 13.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BRUSSELS: Ufaransa kuyatambua mauaji ya Waarmenia kuwa ya kimbali kuazua wasi wasi

Umoja wa Ulaya umeelezea wasi wasi kufuatia kuidhinishwa na baraza la wawakilishi la Ufaransa mswada wa azimio wa kuyatambua mauwaji ya Waarmenia yaliyofanywa na Waturuki mnamo vita vikuu vya kwanza vya dunia kuwa ni ya kuangamiza halaiki ya watu. Mswada huo wa sheria itabidi uidhinishwe pia na baraza la seneti. Lakini tayari umezusha malalamiko. Msemaji wa Halmashauri ya Ulaya, amesema kuwa hatua hiyo ya Ufaransa, itakuwa kizingiti kwa juhudi za kuumaliza mzozo wa miongo kadhaa juu ya swala hilo la mauwaji ya Waarmenia ambapo inakisiwa kuwa watu 1,5 milioni waliuawa. Na nchini Uturuki, kumefanyika maandamano mbele ya ubalozi wa Ufaransa mjini Ankara ya kulaani kupitishwa kwa azimio hilo. Uturuki kwa muda wote ilikanusha kuhusika na mauwaji hayo ikidai kuwa mauaji mengi yalitokea katika vita kati ya wakristu wa Kiarmenia na waislamu wa Kituruki.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com