BRAZZAVILLE: Duru ya pili ya uchaguzi wa Bunge la Kongo | Habari za Ulimwengu | DW | 05.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BRAZZAVILLE: Duru ya pili ya uchaguzi wa Bunge la Kongo

Nchini Jamhuri ya Kongo kunafanywa duru ya pili ya uchaguzi wa bunge.Hii leo ni viti 84 vinavyogombewa katika maeneo 19 ya uchaguzi sehemu za kati na kaskazini ya mji mkuu Brazzzavile.Matatizo mbalimbali yaliyozuka wakati wa duru ya kwanza ya uchaguzi hapo tarehe 24 mwezi Juni yalisababisha uchaguzi huo kufutwa katika maeneo hayo.

Katika duru hiyo ya kwanza viti 50 kutoka jumla ya 53 vilikwenda kwa chama cha Rais Denis Sassou Nguesso alie madarakani tangu miaka kumi pamoja na washirika wake.

Upigaji kura huo ulikuwa na mambo mengi yasio ya kawaida,kama vile kutokamilika kwa orodha ya wapiga kura na kukosekena kwa vyeti vya kupigia kura.Duru ya kwanza ilikosolewa na Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati na vile vile muungano wa mashirika yasio ya kiserikali,ulitoa wito wa kufutilia mbali uchaguzi huo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com