Brassels.Alioyekuwa amefungwa Guantanamo Bay ailaumu Ujerumani na Uturuki. | Habari za Ulimwengu | DW | 23.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Brassels.Alioyekuwa amefungwa Guantanamo Bay ailaumu Ujerumani na Uturuki.

Raia wa Uturuki aliyezaliwa Ujerumani amewalaumu maafisa wa Ujerumani na Uturuki kwa kushindwa kumsaidia kufuatia miaka yake mitano ya kifungo katika jela ya Kijeshi ya Kimarekani ya Guantanamo Bay iliyopo nchini Cuba.

Murat Kurnaz aliyeachiliwa huru mwezi August, ameiambia kamati maalum ya Bunge la Ulaya iliyokutana Brussels kwamba, si Berlin wala Ankara iliyojishughulisha kumtoa katika kifungo huko Guantanamo.

Aidha amewalaumu wanajeshi wa jeshi maalum la Ujerumani kwa kumtendea vibaya nchini Afghanistan kabla hajahamishiwa Guantanamo Bay.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com