Brasilia.Lula da Silva ashinda tena uchaguzi nchini Brazil. | Habari za Ulimwengu | DW | 30.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Brasilia.Lula da Silva ashinda tena uchaguzi nchini Brazil.

Rais wa sasa wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva ameshinda kipindi kingine cha Urais nchini humo.

Lula da Silva ameshinda kwa zaidi ya asilimia sitini ya kura na kumshinda mpinzani wake Geraldo Alckmin katika kile maofisa wanachokiita ni ushindi laini kabisa wa awamu ya pili.

Akisherehekea ushindi wake, Rais Lula ameahidi kujenga misingi imara na bora zaidi nchini Brazil.

Rais Luiz Inacio Lula da Silva ataapishwa tarehe mosi Januari mwakani.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com