1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden na Putin wafanya mazungumzo kwa njia ya mtandao

Sylvia Mwehozi
8 Desemba 2021

Rais Joe Biden amemuonya mwenzake wa Urusi Vladmir Putin wakati wa mazungumzo ya saa mbili kwa njia ya video, akisema kutakuwa na athari kubwa za kiuchumi endapo Urusi itaivamia Ukraine.

https://p.dw.com/p/43yLe
Kombo I Russland Wladimir Putin I USA Joe Biden

Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya White House baada ya mazungumzo hayo, imesema kuwa rais Biden ameelezea wasiwasi wa Marekani na washirika wake wa Umoja wa Ulaya juu ya kuongezeka kwa vikosi vya Urusi vinavyoizingira Ukraine. Taarifa hiyo imeongeza kwamba Biden amesisitiza juu ya kuunga mkono "uhuru wa Ukrainena uadilifu wa maeneo na kutaka kupunguzwa mvutano na kurejea katika njia ya diplomasia.

Kwa upande wa Ikulu ya Urusi Kremlin imeelezea mazungumzo ya Putin na Biden kuwa ya "ukweli" na "kitaaluma" na kuongeza kwamba rais wa Urusi ameiomba Washington itoe dhamana kwamba Jumuiya ya kujihami NATO haitaendeleza upanuzi wake upande wa mashariki.

Akimjibu Biden aliyesema kuwa uwepo wa vikosi vya Urusi karibu na mpaka wa Ukraine ni jambo lenye kutia wasiwasi, Putin amesema Urusi haipaswi kubebeshwa lawama za kuongezeka kwa mvutano. "Ni NATO ambayo inafanya majaribio ya hatari kwa kutumia maeneo ya Ukraine na kuimarisha uwezo wake wa kijesho katika mipaka yetu muhimu", alisema Putin wakati wa mazungumzo yake na Biden. Wakati wa mazungumzo hayo, Putin pia amependekeza kwamba Washington iondoe vikwazo vyote dhidi ya wafanyakazi wa balozi katika nchi zote mbili.

Video-Gipfel von US-Präsident Biden und Russlands Staatschef Putin
Biden akizungumza na Putin kwa njia ya vidioPicha: Adam Schultz/White House/Planet Pix via ZUMA Press Wire/dpa/picture alliance

Msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov amesema katika taarifa yake kwamba "Urusi haijawahi kupanga kumshambulia mtu yeyote", lakini akaongeza kwamba hata wao wana kipimo.

Urusi inakataa madai ya kwamba inapanga kuivamia Ukraine, lakini picha za satelaiti zimeonyesha wanajeshi wengi karibu na mpaka wa Ukraine na kuongeza hofu juu ya kutokea mapigano.

Moscow inayatizama madai ya uvamizi kuwa ya kutia chumvi na badala yake Putin alikusudia kumueleza Biden kwamba ushirikiano wa Ukraine unaozidi kuongezeka na mataifa ya magharibi ni kitisho kwa usalama wa nchi yake. Hiyo ni pamoja na hatua ya Ukraine ya kutaka kujiunga na jumuiya ya kujihami NATO, suala ambalo Moscow inasema halikubaliki. Ingawa mataifa ya Ulaya na Marekani hayataki kutuma vikosi vyake moja kwa moja katika mzozo wa kijeshi na Urusi, njia pekee wanayofikiria na kuishinikiza zaidi Moscow.

Urusi yapongeza mkutano wa Biden na PutinMarekani inasema kwamba inaweza kuiwekea Urusi vikwazo vikali vya kiuchumi, lakini bado haijavitaja. Msemaji wa White House Jen Psaki aliwaeleza waandishi wa habari kwamba wameshauriana na washirika wao na wanaamini kwamba wamo katika njia inayoweza kuanzisha vikwazo vikali vitakavyoathiri uchumi wa Urusi.

Mbali na mgogoro wa Ukraine, Biden na Putin pia wamejadiliana juu ya masuala mengine ikiwemo mpango wa nyuklia wa Iran na wimbi la mashambulizi ya mtandaoni dhidi ya Marekani.