BERLIN:Katibu mkuu mteule Ban Ki Moon azuru Ujerumani | Habari za Ulimwengu | DW | 07.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN:Katibu mkuu mteule Ban Ki Moon azuru Ujerumani

Katibu mkuu mteule wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amefanya mazungumzo na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel mjini Berlin kujadilia maswala mbalimbali yakiwemo mapendekezo ya mabadiliko katika Umoja wa Mataifa.Kulingana na BI Merkel Umoja wa mataifa ni shirika linalohitaji kuwa na msimamo wa pamoja kwasababu ya umuhimu wake ulimwenguni.

Bwana Ki Moon kwa upande wake anaeleza kuwa anaamini Ujerumani itaendelea kuwa na nafasi muhimu katika Umoja huo.Ban Ki Moon yuko katika ziara ya mataifa muhimu wanachama wa Umoja wa Mataifa kabla kuanza rasmi wadhifa wake Januari mosi mwaka ujao.

Koffi Annan anamaliza muda wake kama Kiongozi wa Umoja wa Mataifa wakati huohuo ambapo Ujerumani nayo inachukua uongozi wa Umoja wa Ulaya vilevile kundi la mataifa yaliyostawi kiviwanda G8.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com