BERLIN:Kansela Merkel aitaka Uturuki kuitambua Cyprus na kukubali biashara huru | Habari za Ulimwengu | DW | 06.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN:Kansela Merkel aitaka Uturuki kuitambua Cyprus na kukubali biashara huru

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema Uturuki lazima ichukue hatua katika mzozo wake na Umoja wa Ulaya juu ya kuitambua na kufanya biashara huru na Cyprus ambayo ni mwanachama wa Umoja huo.

Ujerumani inaitaka Uturuki kuiondolea vikwazo vya kibiashara Cyprus lakini Uturuki badala yake inataka vikwazo vilivyowekwa na shirika la biashara duniani WTO dhidi ya Cyprus kaskazini inayodhibitiwa na Uturuki viondolewe kwanza.

Uturuki imekataa kuitambua serikali ya Cyprus ya Ugiriki ambayo kimataifa inawakilisha kisiwa hicho katika Umoja wa Ulaya.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com