BERLIN.Kansela Angela Merkel aadhimisha mwaka mmoja tangu aanze kuingoza Ujerumani | Habari za Ulimwengu | DW | 22.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN.Kansela Angela Merkel aadhimisha mwaka mmoja tangu aanze kuingoza Ujerumani

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel leo amedhimisha mwaka mmoja tangu aanze kuiongoza Ujerumani.

Akizungumza bungeni bibi Merkel aliwaambia wabunge kwamba serikali yake ya mseto itaendeleza mpango wa mabadiliko katika sera zake.

O ton…..Miezi 12 ni muda mrefu katika siasa, utawala na katika vyombo vya habari lakini kuandaa mustakabali wa nchi ni muda mfupi kwa hivyo kazi tuliyopewa na wapigaji kura mwaka mmoja uliopita bado inaendelea, Tunataraji kuongeza nafasi za kazi katika nchi yetu, kuimarisha elimu na kuweka upya msingi wa utajiri wetu.

Kansela Angela Merkel akichangia katika mjadala wa bajeti amesema uchumi wa Ujerumani umekuwa kwa kiwango cha kuridhisha.

Ameyataja yote hayo kuwa ni mafanikio ya serikali ya mseto ya vyama vya Christian na Social Demokratik.

Kuhusu sera za mambo ya nje bibi Merkel amesema kuwa jukumu la majeshi ya Ujerumani katika kikosi cha umoja wa mataifa nchini Lebanon ni la muhimu lakini amepinga pendekezo la Marekani na jumuiya ya NATO la kutaka idadi ya wanajeshi wa Ujerumani huko nchini Afghanistan iongezwe.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com