BERLIN:India yaitaka Ujerumani ilinde raia wake wanaoishi Ujerumani | Habari za Ulimwengu | DW | 22.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN:India yaitaka Ujerumani ilinde raia wake wanaoishi Ujerumani

India imeitaka serikali ya Ujerumani ichukue hatua za kuwalinda raia wa kihindi wanaoishi nchini Ujerumani.

India imesema hayo katika tamko lililotolewa na wizara yake ya mambo ya nje kufuatia mkasa uliotokea jumamosi iiyopita, ambapo wahindi wanane walishambuliwa katika jimbo la Saxony mashariki mwa Ujerumani.

Wahindi hao walishambuliwa na kundi la vijana 50 wa kijerumani wanaotuhumiwa kuwa mafashisti mamboleo.

Wahindi watatu waliumizwa vibaya na wajerumani hao kabla ya polisi kuwasili.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com