BERLIN : Wanajeshi wa Ujerumani kubakia zaidi Pembe Afrika | Habari za Ulimwengu | DW | 11.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN : Wanajeshi wa Ujerumani kubakia zaidi Pembe Afrika

Bunge la Ujerumani Bundestag limepiga kura kuongeza muda wa shughuli za jeshi la Ujerumani Bundeswehr kwa mwaka mmoja zaidi katika operesheni ya kupiga vita ugaidi inayoongozwa na Marekani ijulikanayo kama Dumisha Uhuru.

Hivi sasa wanajeshi wa Ujerumani 330 wanahusika katika kupiga doria kwenye njia za baharini kwenye Pembe ya Afrika. Kuongezwa kwa muda huo kumepita kwa urahisi kutokana na kuungwa mkono na wabunge wa serikali ya mseto ya muungano mkuu ya Kansela Angela Merkel kutoka chama cha Christian Demokrat na Social Demokrat.Pia hoja hiyo imeungwa mkono na chama cha upinzani cha kiliberali cha Free Demokrat.

Chama cha upinzani cha Kijani na kile cha sera za mrengo wa shoto cha Left vimepiga kura dhidi ya hoja hiyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com