1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Uwezekano wa mazungumzo na Iran bado upo

15 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD2n

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani amesema kwamba kwa hivi sasa hana matazamio ya kufikiwa ufumbuzi katika mazungumzo juu ya mpango wa nuklea wa Iran.

Frank Walter Steinmeir amesema jumuiya ya kimataifa ilikuwa inajiandaa kuiwekea vikwazo Iran baada ya uongozi wa nchi hiyo kugoma kuachana na mpango wake huo wa nuklea.Hata hivyo Steinmeir amesema chaguo la kufanyika kwa mazungumzo hayo litaendelea kuwa wazi kwa Iran.

Iran hivi karibuni ilikataa mpango wa vifuta jasho wenye lengo la kuishawishi nchi hiyo kuachana na shughuli zake za kurutubisha uranium.

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya Iran Mohamad Ali Hussein amesema hapo jana kwamba vitisho vinavyotolewa na mataifa ya magharibi kuikewa vikwazo nchi hiyo kutokana na mpango wake tata wa nuklea ni vita tu vya kisaikolojia na kwamba Iran haitishwi na vitisho hivyo na amerudia tena ahadi ya nchi yake ya kuendelea na mpango wake huo wa nuklea.