BERLIN: Ujerumani kuimarisha msaada Afghanistan
5 Septemba 2007Matangazo
Serikali ya Ujerumani ina azma ya kuimarisha juhudi zake za kuijenga upya Afghanistan.Vyombo vya habari vya Ujerumani vimeripoti kuwa mwakani,msaada wa kuijenga upya Afghanistan utaongezwa kutoka Euro milioni 25 kufikia hadi milioni 125.Serikali mjini Berlin,vile vile imesisitiza kuwa itaendelea na wajibu wake kusaidia kuleta utulivu wa muda mrefu katika kanda hiyo.