BERLIN : Ujerumani ipo tayari kuisaidia zaidi Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 11.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN : Ujerumani ipo tayari kuisaidia zaidi Irak

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema, serikali ya Berlin huenda ikaimarisha juhudi za kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Kiiraqi katika vituo vilivyo nje ya nchi hiyo.Wakati huo huo lakini akaongezea kuwa kwa hivi sasa hakuna mipango ya aina hiyo.Merkel alikuwa akizungumza baada ya kukutana na rais Hosni Mubarak wa Misri mjini Berlin.Kansela Merkel alikariri kuwa mwakani,Ujerumani itakapopokea kwa miezi sita wadhifa wa urais wa Umoja wa Ulaya,ataitumia fursa hiyo kufufua juhudi za kutafuta suluhisho la amani kati ya Waisraeli na Wapalestina.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com