BERLIN: Pendekezo la kuwa na sheria kali za uhamiaji | Habari za Ulimwengu | DW | 22.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN: Pendekezo la kuwa na sheria kali za uhamiaji

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Ujerumani,wanafunzi wa kigeni wanaotaka kutembea Ujerumani huenda wakakabiliwa na udhibiti mkali wa visa na ruhusa ya kubakia nchini haitokuwa zaidi ya miaka miwili.Gazeti la “Die Welt” linasema,wizara ya mambo ya ndani ya Ujerumani inatazamia kuwa na sheria kali za uhamiaji, kufuatia majeribio mawili yalioshindwa kufanikiwa ya kutaka kuripua mabomu ndani ya treni Julai iliyopita.Vijana wawili wa Kilebanon na Msyria mmoja wapo kizuizini kuhusika na tukio hilo. Jarida la Kijerumani “Spiegel” linasema,wizara ya ndani inawataka maafisa majimboni kuwachunguza kwa makini zaidi wanafunzi wa kigeni walio Ujerumani.Vile vile wanafunzi hao,wachunguzwe walitokea na wanachosomea.Gazeti la Die Welt linasema,wizara ya ndani inataka pia kutumia utaratibu wa kuchukua alama za vidole vya watu wanaoishi Ujerumani na hutoa dhamana ya kusimamia gharama za wanafunzi wanaokuja kutembea.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com