BERLIN: Mateka mwanamke wa Ujerumani aachiliwa huru | Habari za Ulimwengu | DW | 11.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN: Mateka mwanamke wa Ujerumani aachiliwa huru

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani, Frank Walter Steinmeier, amesema mwanamke wa kijerumani aliyetekwa nyara nchini Irak mapema mwaka huu, ameachiliwa huru.

Waziri Steinmeier amesema Hannelore Krause mwenye umri wa miaka 61 sasa yuko katika ubalozi wa Ujerumani mjini Baghdad.

´Kuzuiliwa kwa Bi Hannelore Krause kwa siku 155 kumemalizika. Tangu jana yuko huru na yuko chini ya ulinzi wa Ujerumani katika ubalizo wetu mjini Baghdad.´

Hata hivyo Frank Walter Steinmeier amesema mtoto wa kiume wa mama huyo, Sinan, bado anazuiliwa na watekaji nyara lakini akaahidi serikali itaendelea kufanya kila inaloweza kumuokoa kijana huyo.

Hannelore Krause na mwanawe, Sinan, walitekwa nyara mnamo tarehe 6 Februari mwaka huu nchini Irak.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com