1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN. Kansela Gerhard Schröder asema ana matumaini ya kushinda uchaguzi

19 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEjn

Kansela Gerhard Schröder wa Ujerumani amesema kwamba upo uwezekano wa yeye kushinda uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.

Kwa sasa kura ya maoni inaonyesha chama cha kansela Gerhard Schröder cha Social Democtratic Party kinafukuzana kwa karibu na chama cha upinzani cha Christian Democrats ambacho kinaongoza kwa pointi 12.

Kansela Schröder amesema kwamba anamatumaini makubwa ya kushinda tena kwani mfumo wa wapinzani wake wa kufufua uchumi wa Ujerumani haukubaliki na wengi.

Iwapo bibi Angela Merkel atashinda uchaguzi wa septemba 18 basi atakuwa mwanamke wa kwanza nchini Ujerumani kuchukua wadhfa wa Ukansela.