BEIRUT:Wagombea walioungwa mkono na serikali washinda uchaguzi | Habari za Ulimwengu | DW | 06.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BEIRUT:Wagombea walioungwa mkono na serikali washinda uchaguzi

Maelfu ya watu nchini Lebanon walishiriki katika uchaguzi uliomalizika hapo jana kuwachagua wabunge wawili watakao chukuwa nafasi ya wawakilishi waliouwawa.

Matokeo rasmi yameonyesha kuwa mgombea anaeiunga mkono serikali mjini Beirut, ameshinda kiti hicho kwa kura nyingi, ilihali mgombea wa upinzani katika jimbo la Metn ameshinda kwa tafauti ndogo ya kura.

Uchaguzi huo ulifanyika chini ya ulinzi mkali.

Wawakilishi wa maeneo hayo walikuwa aliyekuwa waziri Pierre Gemayel aliyeuwawa kwa kupigwa risasi mwezi Novemba mwaka jana na mbunge Walid Eido aliyeuwawa katika shambulio la bomu la kutegwa ndani ya gari la mwezi Juni.

Wote wawili walikuwa wakosoaji wa serikali ya nchi jirani ya Syria na wafuasi wa serikali ya waziri mkuu Fuad Siniora inayopendelewa na nchi za magharibi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com