BEIJING : Mkuu wa shirika la chakula na madawa anyongwa | Habari za Ulimwengu | DW | 10.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BEIJING : Mkuu wa shirika la chakula na madawa anyongwa

Mkuu wa zamani wa shirika la chakula na madawa la China amenyongwa.

Zheng Xiaoyu amehukumiwa adhabu ya kifo baada ya kupatika na hatia ya kupokea hongo kwa ajili ya kuidhinisha matumizi ya mamia ya madawa ambayo baadhi yao yamekuja kuthibitika kuwa ni ya hatari.Wachambuzi wa mambo wanasema kifo cha Zheng kimetakiwa kiwe mfano katika kudhibiti ulimwengu wa shughuli za viwanda vya vyakula na madawa nchini China uliojaa vurugu.

Mifumo ya kudhibiti viwango vya walaji nchini China imekuja kuwa chini ya uchunguzi mkali hivi karibuni ndani na nje ya nchi kutokana na matukio kadhaa kuanzia na madawa ya bandia hadi vyakula vilivyokuwa na sumu ya kemikali.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com