BAGHDAD:Majeshi na Marekani na Iraq yaweka mikakati zaidi kuwakabili wanamgambo huko Baghadad | Habari za Ulimwengu | DW | 08.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD:Majeshi na Marekani na Iraq yaweka mikakati zaidi kuwakabili wanamgambo huko Baghadad

Kamanda wa majeshi ya Marekani nchini Iraq, Generali David Petraeus amesema kuwa wanagambo waasi nchini humo wamezidisha mashambulizi yao.

Akizungumza katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari toka alipochukua jukumu hilo, Mkuu huyo wa majeshi ya Marekani nchini Iraq, amesema kuwa hali hiyo imekuja toka majeshi ya Marekani na yale ya Iraq kuanzisha msako mkali wiki tatu zilizopita.

Maafisa wa kijeshi wanaamini kuwa wanamgambo wengi wa kujitoa mhanga huenda wamehama kutoka Baghdad na kwenda katika maeneo ya jirani kukwepa msako wa majeshi ya Marekani na Iraq.

Marekani imepanga kupeleka askari wa ziada elfu 17 na 500 jijini Baghdad, lakini Generali David amesema kuwa mpaka sasa haoni umuhimu wa kuhitaji askari zaidi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com