BAGHDAD: Irak yajadili kitisho cha Uturuki | Habari za Ulimwengu | DW | 16.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Irak yajadili kitisho cha Uturuki

Waziri Mkuu wa Irak,Nuri al-Maliki ameitisha mkutano wa dharura wa baraza lake la mawaziri kujadili vitisho vya Uturuki inayotaka kupeleka majeshi yake kaskazini mwa Iraq.Siku ya Jumatano,bunge la Uturuki litapiga kura ikiwa liidhinishe mswada wa serikali unaoshauri kupeleka majeshi yake kaskazini mwa Irak,kuwapiga waasi wa Kikurd wa PKK,walio na vituo vyao kaskazini mwa Irak.

Serikali za Irak na Marekani zimetoa mwito kwa Uturuki kutochukua hatua hiyo,zikiwa na hofu kuwa mashambulizi ya aina hiyo huenda yakavuruga hali ya utulivu katika eneo hilo la mpakani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com