Baada ya uchaguzi wa Ujerumani | Magazetini | DW | 29.09.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Baada ya uchaguzi wa Ujerumani

Hatima ya chama cha upinzani SPD ?

default

Angela Merkel (CDU) na mshirika wake G.Westerwelle (FDP)

Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo, yamechambua tena matokeo ya uchaguzi wa Bunge la Ujerumani wa hapo juzi Jumapili na nini cha kutarajia tangu kutoka serikali mpya ya Kanzela Angela Merkel wa chama cha CDU/CSU na mshirika wake Guido Westerwelle wa chama cha kiliberali cha FDP .Pia hatima ya chama kikuu cha Upinzani SPD imezungumzwa.

Uchambuzi wa gazeti la Reutlinger General-Anzeiger kuhusu serikali mpya ya muungano wa vyama vya CDU/CSU na FDP-ile inayoitwa muungano wa bendera nyeusi na manjano unasema:

Serikali ya muungano wa vyama vya vya bendera nyekundu na manjano kwa mwaka huu wa 2009, ni tofauti kabisa na ile ya mfumo kama huo ilioundwa chini ya uongozi wa Kanzela wa zamani Helmut Kohl. Enzi zile, Angela Merkel alikuwa msichana wa Bw.Kohl na kupanda ngazi kuja juu madarakani,zimepita kama zile za mvulana afanyae mzaha- Guido Westerwelle.

Usoni kabisa , Bw. Westerwelle na chama chake cha FDP kilichoimarika kutokana na matokeo ya uchaguzi huu, anaonesha kujiamini hata ni vigumu kulinganisha na chama chake cha wakati ule. Nguvu hizi mpya za waliberali ,zinakumbana na muungano wa vyama vya CDU/CSU ambao ingawa unakamata wadhifa wa kiongozi wa serikali (Kanzela) ,hatahivyo umedhofika kutokana na matokeo ya uchaguzi.....Kwahivyo, washirika wote 2 hawatakirimiana zawadi."

Ama KIELER NACHRICHTEN likiichambua pia serikali ya muungano huu , laandika kwamba, hata ushindi wa waliberali ukiwa mkubwa hivyo,hautoshi kuhalalisha yafanyike mageuzi makubwa ya sera.Jaribio la kuwatia shime wajerumani kufungua masoko zaidi na kujitwika dhamana zaidi,kulishindwa tayari miaka 4 nyuma.Gazeti laongeza:

"Jaribio la pili kufanya hivyo, hakuthubutu kulifanya Bibi Angela Merkel na ndio maana anatafsiri matokeo ya uchaguzi kimsingi, ni hamu ya watu kuendeleza yaliokuwapo.Bila ya shaka, itapasa kufanya marekebisho fulani hasa katika yale yaliokwamishwa na SPD...."

Gazeti la BERLINER MORGENPOST laandika kwamba, hadi sasa Bw.Westerwelle akiwatia watu tamaa.Sasa wakati umewadia kutekeleza aliowaahidi na sio tu kwa fikra,uwezo wa kutekeleza ,bali pia katika kuamua nani anashika wadhifa gani: Gazeti laongeza:

Endapo wakichaguliwa katika Baraza la mawaziri akina Solms na Brüderle au Pieper na Leutheusser-Schnarrenbeger,basi matarajio makuu ya kuanza upya yatatoweka haraka....."

Likigeukia hatima ya chama cha SPD kinachoelekea sasa upande wa upinzani, gazeti la SÄCHSICHE ZEITUNG laandika:

Chama cha SPD kiko njia panda: Wafuasi wake wa mrengo wa shoto ili kurejesha imani yao chamani bila ya wakati huu huo wale wa mrengo wa kati kuwapoteza.Kutimiza shabaha hiyo, chama kitahitaji kigogo imara kileleni na wakati huu hiyo ni bidhaa adimu.Yule ambae hataki kusota katika viti vya upinzani Bungeni,anapaswa jambo moja kutia maanani:Uchaguzi wa Ujerumani ,ushindi unaamuliwa na bawa la kati na hii pia ilikuwa hivyo juzi Jumapili.

Kuhusu hatima ya Bw.Franz Münterfering-mojawapo wa vigogo vya chama ambae muda wake sasa umepita, gazeti la Fuldaer Zeitung laandika:

"Muda wa mzee Munterfering umepita na kudai mambo yaendelea kama yalivyokuwa, hii itakiongoza chama hiki cha kale kaburini.Kwani, miaka 11 ya kuwapo madarakani, SPD kimepoteza utambulisho wake na wapiga kura wamekiadhibu."

Mwandishi:Ramadhan Ali/Dt.Zeitungen

Mhariri:M.Abdul-Rahman