1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfrika Kusini

Afrika Kusini yakataa kuwapokea wakimbizi wa Afghanistan

Daniel Gakuba
2 Septemba 2021

Afrika Kusini imesema imekataa ombi la kuwapokea wakimbizi kutoka Afghanistan, ambao walifika Pakistan wakiukimbia utawala wa Taliban. T

https://p.dw.com/p/3zod6
Deutschland | G20 | Compact with Africa meeting in Berlin | Cyril Ramaphosa
Picha: Tobias Schwarz/REUTERS

Tangazo la wizara ya mambo ya nje mjini Pretoria limesema Afrika Kusini tayari inawapa hifadhi wakimbizi wengi kutoka mataifa mengine, ambapo inawahudumia kwa mafao ya kijamii na matibabu.

Wizara hiyo ilisema katika tangazo lake kuwa serikali ya Afrika Kusini ilipokea ombi la kuwapokea kwa muda wakimbizi hao wa Afghanistan, wakati wakisubiri kupelekwa katika nchi nyingine.

Baadhi ya nchi za Afrika, zikiwemo Uganda na Rwanda, ziliridhia ombi la Marekani la kuwapa hifadhi ya muda wakimbizi kutoka Afghanistan.

Mamia kwa maelfu ya raia wa Afghanistan wameikimbia nchi yao baada ya Wataliban kuchukua hatamu za uongozi, kufuatia kuondoka kwa Marekani na washirika wake walioikalia kijeshi Afghanistan kwa miaka 20 iliyopita.