ACCRA:Viongozi wa Afrika wajiandaa kutoa tamko | Habari za Ulimwengu | DW | 03.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ACCRA:Viongozi wa Afrika wajiandaa kutoa tamko

Viongozi wa afrika wanatarajiwa kutoa tamko juu ya njia mbadala ya kuafuata kuelekea umoja imara, katika siku ya mwisho ya mkutano wao wa siku tatu huko Accra Ghana

Viongozi hao wa afrika waligawanyika katika suala la kuwa na serikali moja ya shirikisho la afrika ambapo wengine walitaka kwanza kuimarishwa kwa taasisi za umoja huo wa afrika.

Rais Abdoulaye Wade wa Senegal, Omar Bongo wa Gabon na Mwai Kibaki wa Kenya ni miongoni mwa waliyoungana na kiongozi wa Libya Kanali Muhammar Gaddafi kutaka kuundwa kwa serikali ya shirikisho.

Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini na Umaru Yar dua wa Nigeria wao kwa upande wao walitaka kuimarishwa kwa taasisi za umoja wa afrika kabla ya kuundwa kwa serikali moja.

Waziri Mkuu wa Ureno Jose Socrates ambaye nchi yake kwa sasa ni kiongozi wa zamu wa Umoja wa Ulaya, alitarajiwa kuhutubia kilele cha mkutano huo, pamoja na kamishna mkuu wa tume ya Ulaya,Jose Manuel Barroso.

Ureno inatarajiwa kuandaa mkutano mkubwa wa viongozi wa Afrika na Ulaya mwezi Desemba mwaka huu, ambapo suala la kuhudhuria kwa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe aliyekatika kizuizi cha kuingia barani Ulaya limetatiza.

Jana Waziri Mkuu huyo wa Ureno Jose Socrates alikataa kuzungumzia iwapo Rais Mugabe ataruhusiwa kuingia Ureno kuhudhuria mkutano huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com