Zelensky yuko ziarani nchini Ufaransa
13 Machi 2026
Matangazo
Mazungumzo hayo yatatuama juu ya kuongeza mbinyo dhidi ya Urusi ili kuilazimisha isitishe vita vilivyoingia mwaka wake wa tano.
Ziara yake inafanyika katika wakati mazungumzo kati ya Ukraine na Urusi yanayosimamiwa na Marekani yamekwama kutokana na vita vilivyozuka baada ya Marekani na Israel kuishambulia Iran.
Kulingana na Ikulu ya Ufaransa, Elysee, viongozi hao wawili watajadili uwezekano wa kuongeza vikwazo vya kiuchumi kwa Urusi hususani kwa kuzilenga meli zake zinazosafirisha mafuta kwa siri.
Mapema wiki hii Ikulu ya Urusi, Kremlin, ilikosoa mpango wa Zelenskykuitembelea Ufaransa ikisema ziara hiyo itatatiza mchakato wa amani unaoendelea na kuzitaja juhudi za kuongeza shinikizo kwa Moscow kuwa "jambo la kipuuzi."