1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelenskiy atua Uturuki kufanya mazungumzo na Erdogan

Sudi Mnette
8 Machi 2024

Rais wa Ukraine Volodmyr Zelenskiy yuko mjini Istanbul kwa mazungumzo na Rais wa Uturuki Reccep Tayyip Erdogan ambaye nchi yake imekuwa na mahusiano mazuri na Kyiv na Moscow na imejitolea mara kadhaa kuwa mpatanishi.

https://p.dw.com/p/4dJuP
Ukraine Kiew 2024 | Selenskyj spricht auf der Konferenz "Ukraine. Jahr 2024"
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy akiwasili 'Ukraine kwa ajili ya mkutano wa mwaka, Februari 25, 2024.Picha: Valentyn Ogirenko/REUTERS

Kulingana na afisa mmoja katika serikali ya Urusi, Erdogan anatarajiwa kushinikiza kuhusiana na mazungumzo ya kusitisha vita vya Urusi nchini Ukraine ambavyo vimeingia mwake wake wa tatu. Mazungumzo ya viongozi hao pia yatajikita katika hatua mpya itakayotoa hakikisho la usalama wa meli za kibiashara katika Bahari Nyeusi. Hayo yakiarifiwa, India imesema imegundua "mtandao mkubwa wa ulanguzi wa binadamu" ambao unawashawishi vijana kuelekea urusi kwa ahadiya kazi, ila wanapofika huko wanalazimishwa kupigana katika vita nchini Ukraine. Idara Kuu ya Upelelezi ya India CBI imesema karibu wanaume 35 wamepelekwa Urusi kupitia mpango huo kufikia sasa. Idadi hiyo ni ya juu ikilinganishwa na ile ya watu 20 iliyokuwa imetolewa na wizara ya mambo ya nje ya India.