1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden: Marekani haitoitenga Ukraine katika vita na Urusi

8 Machi 2024

Rais wa Marekani Joe Biden amesema ni sharti nchi yake iendelee kumuwajibisha Rais Vladimir Putin baada ya Urusi kuivamia Ukraine.

https://p.dw.com/p/4dIhU
Hotuba ya  Biden kwa taifa la  Marekani
Rais wa Marekani Joe Biden akitoa hotuba ya Hali ya Taifa katika bunge la Marekani huko Washington, DC, Machi 7, 2024.Picha: ANDREW CABALLERO-REYNOLDS/AFP

Katika hotuba yake ya hali ya taifa katika bunge la Marekani, Biden amesema Marekani haitoiacha Ukraine. Zaidi amesema "Ukraine inaweza kuizuia Urusi iwapo tutasimama na Ukraine na kuipa silaha za kujitetea. Hicho tu ndicho Ukraine inachoulizia, hawataki kupelekewa majeshi wa Marekani, isitoshe hakuna majeshi ya Marekani katika vita vya Ukraine na ninadhamiria hali iendelee kuwa hivyo. Ila sasa msaada kwa Ukraine unazuiwa na wale wanaotaka tujiondoe kutoka kwenye uongozi wetu wa dunia."Biden vile vile amelaani kauli zilizotolewa na mtangulizi wake Donald Trump kuhusiana na Jumuiya ya Kujihami ya NATO, ambapo alisema hatotoa msaada wowote kwa nchi wanachama wa NATO iwapo Urusi ingeshambulia mojawapo ya nchi hizo.