1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zanzibar: Jumuiya ya MUWAZA-Jee Zanzibar ni nchi?

26 Agosti 2008

Msimamo wa MUWAZA kama Zanzibar ni nchi

https://p.dw.com/p/F5CL
Mji mkongwe wa ZanzibarPicha: DW /Maya Dreyer

Karibuni kumeundwa Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi ngambo inayoitwa MUWAZA, yaani Mustakbali wa Zanzibar. Kwa mujibu wa waasisi, malengo ya jumuiya hiyo ni kuwaunganisha Wazanzibari wote ili kuleta utambulisho wa Wazanzibari na kuleta suluhu baina yao pamoja na kupigania mustakbali wa Zanzibar kama nchi, kwa ujumla, na kulinda maslahi ya kidola, kitaifa na kulinda uhuru wake. Jumuiya hiyo imetangaza kwamba itakuwa na mkutano wake mkuu mwishoni mwa mwaka huu mjini London.

Othman Miraji alizungumza kwa njia ya simu na kiongozi wa waasisi wa jumuiya hiyo, Dr. Yusuf Saleh Salim, aliyoko katika mji mkuu wa Denmark, Copenhagen, kutaka kujuwa kitu gani kilichowachochea kuiazisha jumuiya hiyo wakati huu...