Yaliyohanikiza magazetini hii leo nchini Ujerumani | Magazetini | DW | 04.04.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Yaliyohanikiza magazetini hii leo nchini Ujerumani

Hatima ya mahabusi wawili wa kijerumani nchini Irak na hali nchini Afghanistan

Likiandika kuhusu hatima ya mahabusi wa Ujerumani gazeti la SCHWERINER VOLKSZEITUNG linasema “ni kurushana roho tuu huku” hasa kwa kua kanda ya pili ya video imetolewa muda mfupi baada ya madage ya kijeshi Tornados kuondoka Ujerumani kuelekea Afghanistan.Gazeti linaendelea kuandika:

“Haikua bahati nasibu,wamefanya maksudi kutoa kanda hii ya video wakati huu-ili kuzidi kuwashinikiza wajerumani.Kamati ya wizara ya mambo ya nchi za nje inayoshughulikia mizozo inabidi ifanye kila liwezekanalo ili kuikuza fursa ya kuwakomboa salama usalimini mahabusi hao.Katika kadhia mbili za mwanzo za mahabusi wa kijerumani,mambo yalikwenda vizuri.Lakini licha ya juhudi zote hizo,hakuna kisichokua na kikomo.Serikali kuu ya Ujerumani isikubali hata kidogo kutiwa kishindo na wafuasi wa itikadi kali ya dini ya kiislam,kama ilivyofanya dhidi ya magaidi wa RAF.”Linasisitiza gazeti la SCHWERINER VOLKSZEITUNG.

Gazeti linalochapishwa mjini DORTMUND-WESTFÄLISCHE RUNDSCHAU linahisi:

„Kwa bahati mbaya ni ishara chache tuu zinazoashiria kwamba wateka nyara wanataka fedha tuu.Mengi yanaonyesha kana kwamba wanataka kuishinikiza kisiasa serikali ya mjini Berlin.Kwasababu suala la Ujerumani kujitenga au kuyapa kisogo mapambano dhidi ya ugaidi,halimo kabisa katika ajenda. Kuendelea kufuata mkondo wa busara na wakati huo huo kuyaokoa maisha ya mahabusi wa kijerumani ndio muongozo ambao Berlin inabidi kuufuata,“linahisi gazeti la WESTFÄLISCHE RUNDSCHAU.

„Hoja za wateka nyara zimebadilika kidogo“,linaandika gazeti la SÜDWEST-PRESSE la mjini ULM:

„Patashika hii inamfanya mtu aamini hawa si wateka nyara walioshawishiwa kisiasa,wasiochelea kitu- ni makundi ya wahalifu ambao hawana kazi isipokua kuwasumbua wageni ili wapate fedha.Hawachelei hata kuchochea mgogoro kati ya wananchi na serikali kuu ya shirikisho.Kwa bahati nzuri hawana njia.Lakini isisahauliwe hata magengi ya wahalifu wanawauwa wahanga wao-linakumbusha gazeti la SÜDWEST-PRESSE.

Mada ya pili magazetini hii leo inahusu pendekezo la mwenyekiti wa chama cha Social Democratic-SPD KURT BECK la kushirikishwa baadhi ya wataliban katika mazungumzo ya kuijenga upya Afghanistan.Kuhusu fikra hiyo,gazeti la FRANKFURTER RUNDSCHAU linaandika:

“Kimsingi Beck kasema la maana.Ikiwa watu watataka kuepusha vita vyengine vya wenyewe kwa wenyewe,basi hakuna budi isipokua kuzichanganya upya karata-Kama ilivyokua wakati wa mkutano wa Petersburg karibu na Bonn.Njia iliyobuniwa wakati ule imenza zamani kuwekewa suala la kuuliza-kwasababu kuna wengi ambao hawakutiliwa maanani.Kama mtu anaweza kuwaita wataliban wanaofuata nadharia za wastani?Ni shida kujua imekwenda kwendaje hata Bewck akawaita hivyo.Pengine amekuja na kile ambacho wanaoongoza wizara ya mambo ya nchi za nje wamekua wakikifikiria-linaandika gazeti la Frankfurter Rundschau.

 • Tarehe 04.04.2007
 • Mwandishi Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHTK
 • Tarehe 04.04.2007
 • Mwandishi Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHTK