1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yaliyoandikwa magazetini Ujerumani hii leo

oummilkheir27 Oktoba 2004

Hukumu ya korti kuu ya katiba kuhusu ruzuku kwa vyama vya kisiasa,juhudi za kusaka ridhaa ya wafuasi wa chama cha Christian Democratic katika jimbo la kusini la Baden-Württemberg juu ya nani ashike nafasi itakayoachwa na waziri mkuu Erwin Teufel na mbinu za mawaziri wa fedha wa umoja wa Ulaya ni miongoni mwa mada muhimu zilizochambuliwa na magazeti ya Ujerumani hii leo.

https://p.dw.com/p/CHPD

Korti kuu ya katiba imebatilisha sheria iliyokua ikipiga marufuku misaada ya fedha kutolewa kwa vyama vidogo vidogo ikihoji sheria hiyo inavidhulumu vyama hivyo.Kuhusu mada hiyo gazeti la MANNHEIMER MORGEN linaandika:

"Hukumu ya mahakimu wa mjini Karlsruhe inajitokeza kua funzo katika fani ya demokrasia.Kwasababu,kuundwa vyama vya kisiasa na kua na uwezo wa kushindana katika majukwaa ya kisiasa bila ya pingamizi,ni misingi inayodhaminiwa na kutukuzwa na sheria msingi.Kujaribu kushawishi muundo wa kisiasa,kama inavyodhihirika katika suala la namna ya kutolewa misaada ya fedha kwa vyama vidogo vidogo,ni kinyume na sheria na inaiendeya kinyume pia misingi ya nafasi sawa kwa vyama vyote.Ufanisi wa mbilikimo ni pigo kwa wababe."

Hoja kama hizo zimetolewa pia na gazeti la mjini Postdam la MÄRKISCHE ALLGEMEINE:Gazeti linaandika:

"Kwa kupitisha uamuzi unaoshadidia umuhimu wa mashindano ya kisiasa,mahakimu wamewatahayarisha wale wanaopendelea sheria mpya kuhusu misaada ya fedha kwa vyama vya kisiasa.Hazina uzito hoja kwamba misaada ya fedha inayotolewa ishurutishwe na chaguzi ngapi zinaitishwa au hoja kwamba sheria hiyo mpya itasaidia kuvizuwia vyama vya siasa kali visijiimarishe kutokana na misaada ya na serikali.

Uzito lakini unakutikana katika hoja kuhusu demokrasia:Korti kuu ya katiba mjini Karlsruhe inahisi:njia ambayo tokea hapo ni nyembamba ya kuingia katika soko la kisiasa,haistahiki kuzidi kuwekewa pingamizi."

Nalo gazeti la NORDBAYERISCHE KURIER la mjini Bayreuth,kusini mwa Ujerumani linaandika:

"Wababe wanabuni sheria ili kuzidi kujinufaisha katika nyanja za mashindano ya kisiasa.Wanataka kuwazuwia mbilikimo wasipatiwe misaada ya fedha ya serikali, wao lakini wanajikingia isiyo kidogo.Fedha hizo zilizozuwiliwa zingerejea katika makasha ya makundi yenye nguvu.Imekua bora korti kuu ya katiba imemaliza udhia.Bila ya hivyo,wababe wangeendelea kuamini taifa linamilikiwa na vyama vuikubwa vikubwa.Sivyo hivyo lakini.

Kuhusu kuulizwa maoni yao wanachama wa Christian Democratic Union-CDU katika jimbo la kusini la Baden Württemberg,gazeti la mjini München Südddeutsche Zeitung linaandika:

"Wanachama wa CDU katika jimbo la Baden-Württemberg wanabidi wachague kati ya Annette Schavan na Günther OETTINGER:Katika kundi la Oettinger watu wanang’unika na kujiuliza kwanini ushindi uliokua hakika unawekea suala la kuuliza hivi sasa…Hakuna lakini njia nyengine......Oettinger na Schavan wanabidi wadhihirishe vipi wanafikiria kuongoza na sio tuu kushindana nani akabidhiwe uongozi.

Gazeti la OFFENBURGER TAGESBLATT linachambua:

"Hakuna aliyekua akiamini kwamba chama cha Christian Democratic kitafika hadi ya kuuliza maoni ya wanachama wake.Chama hiki ,ambacho kwa kawaida daima kimekua kikipinga kuwahusisha wafuasi wake,hii leo kinawataka wafuasi wake waachague wanamtaka nani kati ya waziri wa utamaduni Annette Schavan na mkuu wa kundi la CDU Günther OETTINGER,kushika nafasi ya waziri mkuu Erwin Teufel atakapoacha madaraka yake april 19 ijayo.Hakuna uamuzi bora kuwapita Schavan na Oettinger.

Gazeti la PFORZHEIMER ZEITUNG linaonya:

"Bado kuna tokota ndani ya chama cha CDU jimboni Baden Württemberg.Bado makundi hayajaanza kuundwa.Kila siku inayopita hadi kuifikia siku ya kuwauliza wanachama maoni yao,inatishia kuzusha vishindo.Wala isitokee kwamba CDU inashindwa kumpata mmoja kati ya watetezi hao wawili.Lakini suala hasa linalojitokeza ni jee nini kitatokea ikiwa wanachama wa CDU watashindwa kumchagua mmoja kati ya hao wawili,nani atakabidhiwa nafasi ya Erwin Teufel?