Waziri wa maendeleo wa Ujerumani awakumbuka watu waliokufa kutokana na mafuriko ya Sunami huko Indonesia. | Habari za Ulimwengu | DW | 17.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Waziri wa maendeleo wa Ujerumani awakumbuka watu waliokufa kutokana na mafuriko ya Sunami huko Indonesia.

Jakarta:

Waziri wa maendeleo ya kiuchumi wa Ujerumani, Bibi Heidemarie Wieczorek-Zeul, wakati akifanya ziara katika jimbo la Aceh huko Indonesia amewakumbuka watu waliokufa kutokana na janga la mafuriko ya Sunami miaka miwili iliopita. Aliweka shada la mauwa katika kaburi la pamoja karibu na mji mkuu wa jimbo hilo, Bandar Aceh. Katika jimbo hilo huenda zaidi ya watu 170,000 walikufa kutokana na mafuriko hayo ya bahari. Bibi Wieczorek-Zeul aliahidi kwamba Ujerumani itatoa Euro nyingine milioni 20 kusaidia katika ujenzi mpya wa jimbo hilo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com