Waziri mpya wa Uchumi Ujerumani | Matukio ya Kisiasa | DW | 09.02.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Waziri mpya wa Uchumi Ujerumani

Karl Theodor zu Guttenberg anamrithi Michaeol Glos aliejiuzulu kama Waziri wa Fedha wa Ujerumani.Kinachoshangaza ni jinsi mwanasiasa huyo mwenye miaka 37 alivyopanda ngazi haraka na kushika wadhifa kama huo serikalini.

** ARCHIV ** Karl-Theodor zu Guttenberg, Generalsekretaer der Christlich Sozialen Union (CSU), verfolgt am 30. Oktober 2008 eine Pressekonferenz im bayerischen Landtag in Muenchen. Karl-Theodor zu Guttenberg wird Nachfolger von Bundeswirtschaftsminister Michael Glos. Dies erfuhr die Nachrichtenagentur AP am Montag, 9. Februar 2009, aus Unionskreisen. (AP Photo/Christof Stache) ---- Karl-Theodor zu Guttenberg, new Secretary General of the German Christian Social Union Party (CSU), follows a news conference in the Bavarian parliament in Munich, southern Germany, on Thursday, Oct. 30, 2008. (AP Photo/Christof Stache)

Waziri mpya wa Uchumi wa Ujerumani Karl-Theodor zu Guttenberg.

Karl-Theodor zu Guttenberg ana uso wa kupendeza,mwili wa mwanariadha na nywele zilizochanwa nyuma.Yeye ni mwerevu na ana mwendo wa haraka. Alizaliwa tarehe 5 mwezi wa Desemba mwaka 1971 katika familia ya kifalme.Lakini hayo sio yaliyopelekea kuchaguliwa kuwa Waziri wa Uchumi wa Ujerumani.

Mwanasiasa huyo kijana amesomea sheria na siasa na amefaulu vizuri mitihani yake hadi kupata shahada ya udaktari katika fani ya sheria.Anaijua thamani yake na ni mtu mwenye maoni huru kama ilivyodhihirika pale mwenyekiti wa chama chake cha CSU Horst Seehofer alipoingilia kati hotuba ya zu Guttenberg aliekuwa akieleza kuwa Ujerumani hivi sasa inajikuta katika mzozo. Seehofer akaingilia kati na akasema " mzozo wa uchumi na fedha".Hapo zu Guttenberg akamjibu hilo ndio alilotaka kusema pia.

Akiendelea na hotuba yake alisema,dhana hukabiliwa vyema zaidi kwa vitendo,hivyo ndivyo alivyolelewa. Yeye anataka kutumikia taifa na umma - na sio kugeuka karagosi.Amesema,anapokea wadhifa wake mpya kwa heshima na akaongezea kuwa baadhi ya mambo atafanya tofauti na mtangulizi wake Michael Glos.

Akiendelea waziri mpya wa uchumi alisema,yeye binafsi alikuwa na dhamana ya kiuchumi ambako maadili kama vile umuhimu wa masoko huria, mashindano ya kibiashara yanayoruhusiwa,maadili ya kimsingi kama miliki, yote yanaweza kutumiwa kama vipimo vya kibiashara.

 • Tarehe 09.02.2009
 • Mwandishi S.Kinkartz - (P.Martin)
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GqRi
 • Tarehe 09.02.2009
 • Mwandishi S.Kinkartz - (P.Martin)
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GqRi
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com